Bonde La Pangani: Uchambuzi wa Hali Halisi (Toleo la pili)

Madhumuni ya toleo la kwanza la Uchambuzi ya Hali ya Bonde la Mto Pangani yalikuwa kuainisha rasilimali za asili zilizomo katika Bonde hilo, matukio yanayoziathiri na kutambua maeneo ya kufanyia kazi. Madhumuni mengine yalikuwa kutambua mashirika, asasi na wadau wengine ambao IUCN ingeweza kushirikiana nao.

Madhumuni ya toleo la kwanza la Uchambuzi ya Hali ya Bonde la Mto Pangani yalikuwa kuainisha rasilimali za asili zilizomo katika Bonde hilo, matukio yanayoziathiri na kutambua maeneo ya kufanyia
kazi. Madhumuni mengine yalikuwa kutambua mashirika, asasi na wadau wengine ambao IUCN ingeweza kushirikiana nao.

Lengo la WANI ni kuhakikisha kwamba suala zima la ikolojia linazingatiwa katika sera, mipango, na usimamizi wa mabonde ya mito. Katika maeneo ya mabonde ya kufanyia maonyesho yaliyoteuliwa duniani, WANI imepania: kuonyesha namna ya kusimamia mfumo ikolojia, kuwawezesha wananchi kushiriki katika usimamizi endelevu wa rasilimali za maji, kuendeleza usimamizi bora wa vyanzo vya maji na ardhioevu, kuanzisha na kutumia nyenzo za kiuchumi na vivutio, kuongeza maarifa ya kusaidia kufikia maamuzi na kutoa mafunzo yatakayoleta mwamko wa matumizi bora ya maji.

Kufuatia mashauriano na wadau katika Bonde na kwa kuzingatia maazimio ya warsha iliyoendeshwa na Ofisi ya Maji ya Bonde la Pangani (PBWO) kwa ushirikiano na IUCN - Shirika la Kimataifa la Kuhifadhi Uasili iliyofanyika Moshi, Tanzania, kuanzia tarehe 8 hadi 10 Mei, 2002, Bonde la Mto Pangani nchini Tanzania na Kenya lilichaguliwa kuwa eneo la maonyesho la WANI.

Ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za mradi wa maendeleo katika Bonde la Mto Pangani, IUCN ilimwajiri Mshauri Mtaalamu Dk. Kim Geheb, kufanya Uchambuzi wa Hali halisi ya bonde hili. Kazi za ugani kwa ajili ya uchambuzi wa hali halisi zilifanyika mwezi Novemba, mwaka 2002, na ilihusisha mahojiano na wadau mbalimbali katika bonde. Vyanzo vya ziada vya taarifa vilikuwa ni marejeo ya machapisho pamoja na mjadala wa warsha iliyotajwa hapo juu, iliyojulikana kwa jina la “Bonde la Mto Pangani: Usimamizi Shirikishi”

Other Resources and Highlights

Partners and Sponsors

Our Contacts