Mto Pangani Na Mfumo Wake: Ripoti ya Hali ya Bonde

Ripoti hii ya Hali ya Bonde inaeleza kwa muhtasari mambo muhimu yaliyojitokeza katika tafiti hizi za kitaalamu kwa ajili ya watu kwa ujumla. Inaweka msingi wa uelewa wetu wa hali ya sasa ya uhai na kazi mbalimbali zitokanazo na mto Pangani na mfumo wake.

Ripoti hii ya hali ya Bonde imetayarishwa ikiwa ni sehemu ya Tathmini ya Hali ya Maji ya Mradi wa Usimamizi wa Bonde la Mto Pangani. Madhumuni ni kukusanya na kusanisi taarifa zote zinazofahamika hivi sasa juu ya mfumo wa Bonde la Mto Pangani na watumiaji wake, na kusaidia kukuza mtazamo wa usimamizi wa pamoja kwa kuhusisha sekta mbalimbali katika maamuzi ya ugawaji wa maji kwa siku za baadaye. Mtazamo huu unafahamika kama Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Maji.

Katika kutekeleza kazi hii wataalamu wa Ki-Tanzania na wa Kimataifa wamefanya kazi kwa pamoja katika kipindi cha 2005 2006 kuendeleza uelewa wa haidrolojia (muda na kiwango cha mtiririko wa maji) wa Bonde zima la Mto Pangani, maumbile yake, kemikali na biolojia asilia na hali ya uhai wa mfumo wa ki-ikolojia ya mto na umuhimu wa mto kwa maisha na ustawi wa jamii.

Ripoti hii ni muhtasari wa ripoti sita za kifundi ambazo zimekwishaandikwa na Timu ya wataalamu. Ripoti hizo ni kama ifuatavyo: Haidrolojia ya Bonde la Mto Pangani, Ripoti ya Michoro na Ramani, Ripoti ya kuwezesha kuchagua aina za miradi ya maendeleo inayofaa, tathmini ya hali ya uhai wa mto, tathmini ya hali ya uchumi na ustawi wa jamii.

Ripoti hii inaelezea kuhusu hali na mfumo wa mto katika mwaka 2006 kwa kipindi cha kiangazi na masika na inabainisha maeneo muhimu ya kuangaliwa ya mfumo mzima wa mto, Lango la mto na maeneo ya ardhioevu makuu. Aidha, inaonyesha uhusiano kati ya mto na watu ndani ya Bonde, inaelezea maisha yao na inaanza kutambua jinsi viumbe vinavyoguswa na mabadiliko ya hali ya mtiririko wa maji ya mto na mfumo ikolojia.

Other Resources and Highlights

Partners and Sponsors

Our Contacts